

Inactive· since Jul 4, 2026
- 16
- days it ran
- 0
- relaunches
Ad copy
■ SIKU 20 ZA UBATIZO, MWEZI WA JUNI, 2026 - KANISA LA FGBF DAR-ES-SALAAM ■ NI MWEZI WA UINJILISTI ULIOANZA JUMAMOSI, 6.6.2026 HADI LEO IJUMAA, 3.7.2026 ■ NI UBATIZO WA MAJI TELE (YOHANA 3:23) ■ Mahali lilipo Kanisa katika Jiji la Dar-Es-Salaam, Tanzania: BARABARA YA SAM NUJOMA, MWENGE; MKABALA NA MLIMANI CITY AGIZO KUU la Yesu Kristo, siyo tu linamwagiza kila mtu aliyeokoka, kuhubiri Injili kwa kila kiumbe (MARKO 16:15); bali pia, Yesu Kristo, anatuamuru sisi sote tuliookoka, kuzingatia kuwa, wale wote tunaokuwa tumewahubiria Injili, na wakaiamini; au wakaamua kumpokea Yesu, na kupewa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu (YOHANA 1:12); tunatakiwa kuhakikisha kwamba, watu hao WANAOAMINI, WANABATIZWA (MARKO 16:16), UBATIZO WA MAJI TELE (YOHANA 3:23); yanayotosha kumwezesha mtu aliyeamini, kuzikwa pamoja na Yesu katika Ubatizo huo; unaokuwa kama, "Kaburi la Maji"; na kufufuka pamoja naye: WAKOLOSAI 2:12, "MKAZIKWA PAMOJA NAYE KATIKA UBATIZO; NA KATIKA HUO MKAFUFULIWA PAMOJA NAYE, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu." Angalia pia, WARUMI 10:9; na WARUMI 6:4. Ubatizo wa Maji Tele, ni tendo (YAKOBO 2:17-26), au jibu; linaloonyesha kwamba, mtu huyo aliyemwamini Yesu; ana dhamiri safi mbele za Mungu (1 PETRO 3:21), au ana nia thabiti ya kuitimiza haki yote (MATHAYO 3:13-15), yaani, ana nia thabiti, ya kuyatimiza maagizo yote ya Mungu; kwani, maagizo yake yote ni ya haki (ZABURI 119:172); na pia, ana nia ya kufuata kielelezo au nyayo za Yesu Kristo. Aidha, inatupasa kuwafanya wote hao waliomwamini Yesu, kuwa Wanafunzi wa Yesu; na pia kuhakikisha wanafundishwa KUYASHIKA YOTE aliyotuamuru Yesu Kristo (MATHAYO 28:19-20; 3:13-17; YOHANA 13:15; 1 PETRO 2:21). Kwa sababu hii, sasa; Washirika wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Dar-Es-Salaam; lililoko Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge; HAWAISHII TU KATIKA KUFANYA KAZI YA KUWAHUBIRIA WATU INJILI, HUKO MITAANI; bali mapema sana, huwafuatilia wale waliompokea Yesu, baada ya kuhubiriwa; na kisha kuwafundisha Somo, "MTIHANI WA KWANZA WA UTII KWA WATOTO WA KUTII"; ambalo huwafundisha na kuwaongoza watu ambao wanakuwa wametubu kwa dhati dhambi zao, au uasi wao; na kugeuzwa kutoka katika hali ya kuwa wana wa kuasi, au wana wa uasi; na kufanyika kuwa WATOTO WA KUTII (MITHALI 28:13; 1 YOHANA 3:4; WAEFESO 2:1-2; 5:6; 1 PETRO 1:14); katika kutekeleza wajibu wao wa kubatizwa katika Maji Tele; mapema iwezekanavyo (ZABURI 119:60). Hivyo basi, kwa jinsi ileile ambavyo Washirika wa Kanisa hili, wanavyohubiri Injili mitaani, kwa siku kadha wa kadha, KILA WIKI; vivyo hivyo, Siku za Ubatizo, nazo huwa kadha wa kadha, KILA WIKI; katika Mwezi husika wa Uinjilisti. Kwa hiyo, basi; kwa kuzingatia maelezo yaliyokwisha kuelezwa hapo juu; LEO, Siku ya IJUMAA, tarehe 3.7.2026; Ubatizo wa Maji Tele, umefanyika kwa AWAMU TATU TOFAUTI, katika Kanisa la FGBF DAR-ES-SALAAM; ikiwa ndiyo kilele cha MWEZI HUU WA UINJILISTI, wa Kanisa hili; ulioanza JUMAMOSI, tarehe 6.6.2026, hadi leo IJUMAA, tarehe 3.7.2026. Shughuli hii, ndiyo shughuli ya kawaida ya kila Siku ya Kilele cha Mwezi husika wa Uinjilisti, ambayo huwa ni Siku ya IJUMAA ya kwanza ya mwezi, kama ya leo. Siku hii ya Ijumaa, hufanyika SEMINA TATU TOFAUTI ambazo huambatana na AWAMU TATU TOFAUTI ZA UBATIZO; yaani Ubatizo hufanyika mwisho wa Semina ya Kwanza; halafu hufuatia Semina ya Pili na Ubatizo wake; na kisha Siku hii, huhitimishwa kwa Semina ya Tatu na Ubatizo wake. Shughuli hii nzima ya Siku ya Kilele cha Mwezi wa Uinjilisti, HUANZA SAA 3 ASUBUHI, HADI SAA 3 USIKU. Sasa basi, katika Mwezi huu wa Uinjilisti, kwa ujumla wake; makumi kwa makumi ya watu, wamebatizwa, katika SIKU 20 TOFAUTI, za Mwezi huu wa Uinjilisti. Picha hizi ni za BAADHI ya watoto hao wa kutii (1 PETRO 1:14), waliobatizwa katika BAADHI ya Siku hizo. Siku hizo 20 tofauti, ambapo Ubatizo wa Maji Tele, ulifanyika, katika Mwezi huu wa Uinjilisti; zilikuwa kama ifuatavyo: Jumamosi 6.6.26; Jumapili 7.6.26; Jumanne 9.6.26; Jumatano 10.6.26; Alhamisi 11.6.26; Ijumaa 12.6.26; Jumamosi 13.6.26; Jumapili 14.6.26; Jumatatu 15.6.26; Jumatano 17.6.26; Alhamisi 18.6.26; Jumamosi 20.6.26; Jumapili 21.6.26; Ijumaa 26.6.26; Jumamosi 27.6.26; Jumapili 28.6.26; Jumatatu 29.6.26; Jumanne 30.6.26; jana Alhamisi 2.7.26; na leo Ijumaa 3.7.26. Hivyo basi, leo, ndiyo kilele cha Ubatizo huo, ambao umekuwa ukifanyika siku kadha wa kadha, kila wiki. Tunapenda kuchukua nafasi hii, kumshukuru sana, BWANA WA MAVUNO, ROHO MTAKATIFU (MATHAYO 9:38; MATENDO YA MITUME 13:2); ambaye bila Yeye, kazi hii yote isingewezekana; na tena tunawapongeza watoto wote wa kutii, waliobatizwa siku yoyote ile, katika Mwezi wote huu wa Uinjilisti; na vilevile tunawapongeza pia, watendakazi wote WALIOWAHUBIRIA INJILI MITAANI, hadi wakakata shauri kutubu dhambi zao kwa kumaanisha kuziacha (MITHALI 28:13; MARKO 1:14-15; MATENDO YA MITUME 3:19; 5:31; 17:30; 26:20), na kuokolewa; na tena tunawapongeza sana watendakazi wote waliowafundisha somo, "MTIHANI WA KWANZA WA UTII, KWA WATOTO WA KUTII", hadi wakaamua kubatizwa. Vilevile, tunazipongeza Zoni zote zilizoweza kufikia malengo yao yaliyowekwa; na zaidi sana Zoni zile ambazo zimevuka malengo yao yaliyowekwa. Na bila kusahau, tunawapongeza pia wanamaombi walioiombea kazi hii yote, mchana na usiku; kwa mwezi mzima huu. Kwa hakika, kila mtendakazi atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe (1 WAKORINTHO 3:8). Watendakazi wote, sasa tujipange upya kuitenda kazi hii ya thamani kubwa, yenye ijara au mshahara utakaodumu milele na milele; tofauti na ajira za hapa duniani, zenye ijara au mshahara usiodumu (YOHANA 4:35-36; 2 MAMBO YA NYAKATI 15:7; WAKOLOSAI 3:23-24; WAEBRANIA 10:34-35; 1 WAKORINTHO 15:58; 2 WAKORINTHO 4:18); kwa bidii na juhudi kubwa zaidi (WARUMI 12:11); katika Mwezi mpya wa Uinjilisti, unaoanza kesho Jumamosi, tarehe 4.7.2026; na kufikia kilele chake Ijumaa, tarehe 7.8.2026; huku tukikumbuka kwamba IMETUPASA kuzitenda kazi zake Mungu wetu, maadamu ni mchana; usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi (YOHANA 9:4). MARANATHA!!!
Like this ad? Make it yours.
Crush rebuilds this exact creative around your product — your brand, your colors, your offer — in about a minute.

